Mnyambuliko wa Vitenzi

Mnyambuliko wa vitenzi ni jinsi vitenzi vinavyobadilika kulingana na kauli/hali mbalimbali. Kwa mfano kutokana na kitenzi 'soma' tunawezapata somea, somewa, somwa n.k.
Ni vizuri kuelewa kwamba sio vitenzi vyote vinavyonyambulika katika kila kauli.

Kwa sasa tutaangalia kauli zifuatazo. Ili kukusaidia uelewe kauli hizi vizuri, tutakutumia wewe kama mfano na mtu mwengine; lakini mnyambuliko unaweza kutumika kwa kitu chochote kila. :

  1. Kauli ya Kutenda - kitendo katika hali yake ya kawaida (bila kunyambuliwa)
  2. Kauli ya Kutendea - kufanya kitendo kwa niaba(au kwa ajili) ya mtu mwengine
  3. Kauli ya Kutendana - unamfanya mtu kitendo, naye anakufanya vivyo hivyo
  4. Kauli ya Kutendena - unafanya kitendo kwa niaba mtu, naye anafanya kitendo hicho kwa niaba yako.
  5. Kauli ya Kutendwa - kuathirika moja kwa moja na kitendo
  6. Kauli ya Kutendewa - kitendo kufanywa kwa niaba yako au kwa ajili yako.
  7. Kauli ya Kutendeka - kitendo kukamilika au kuwa katika hali timilifu
  8. Kauli ya Kutendesha - kumfanya mtu atende jambo fulani
  9. Kauli ya Kutendeshana - mtu anakufanya utende jambo fulani, nawe unamfanya atende jambo lilo hilo

Mifano Katika Jedwali

TENDATENDEATENDANATENDEANATENDWATENDEWATENDEKATENDESHATENDESHANA
fanyafanyiafanyanafanyianafanywafanyiwafanyikafanyishafanyishana
LimaLimiaLimanaLimianaLimwaLimiwaLimikaLimishaLimishana
PikaPikiaPikanaPikianaPikwaPikiwaPikikaPikishaPikishana
LiaLilia?Liliana?LiliwaLilikaLizaLizana
kulalialanalianaliwaliwalikalishaLishana
pendapendeapendanapendeanapendwapendewapendekapendezapendezana
ombaombeaombanaombeanaombwaombewaombekaombezaombezana
tembeatembeleatembeleanatembeleanatembelewatembelewatembelekatembezatembezana
abuduabudiaabudianaabudianaabudiwaabudiwaabudikaabudishaabudishana

Hivi karibuni tutakuletea mnyambuliko katika kauli za kutendua, kutendeshea, kutendesheana, kutendata,
kutendama n.k. Isitoshe tutakuletea mnyuambuliko wa vitenzi vya silabi moja.