Sauti za Kuimba

Sauti za Kuimba is the largest library of songs from East African Catholic community. Nyimbo za kwaya mbalimbali za kikatoliki kutoka Afrika Mashariki.

Sauti za KuimbaSauti za Kuimba ni talanta tumepewa na Mungu tumwimbie

Ni talanta, tutumie watu waokolewe, wauone uso wa Mungu

Tuwafariji waombolezao, tuwape tumaini walokata tamaa

Tuwateteee wasio na mtetezi, walionyamazishwa na kelele za dunia

Tuwaburudishe waliozubazwa na taabu za dunia


Sauti za Ngoma. Sauti ya kinanda. Sauti ya kinubi. Sauti ya kayamba. Sauti ya zeze. Sauti za Ala Zote za Muziki. Pamoja na sauti tamu tulizojaliwa. Hizi ni Sauti za Kuimba.
Request for Lyrics here.


Kinukuu Teule

Yesu mwema najitolea kwako

kwa leo hii na siku zote

Nafsi yangu na moyo wangu wote

Heri kweli, heri kweli, heri kweli raha ya uwingu

Heri kweli, heri kweli, heri kweli raha ya uwingu


Yesu Mwema najitolea Kwako - F. Malema L. Mwanampepo


Hubirini kwa Sauti ya Kuimba, tangazeni haya, yatamkeni mpaka mwisho wa dunia